ATAPE NI NINI ?

Ni kifupisho cha Association of Tanzanian Adventist Professionals and Entrepreneurs.

Hiki ni Chama cha kikanisa cha wanataaluma na wajasiriamali ndani ya kanisa la Waadventista Wa Sabato. Chama hiki kilianzishwa rasmi mwaka 2002 na kinatambulika na kuendesha shughuli zake za kuunga mkono harakati za kutimiza utume wa kanisa la Waadventista Wa Sabato ulimwenguni.

Washiriki wote waliojaliwa kuwa na taaluma yo yote, au ujuzi wo wote au maarifa ya kazi Fulani, Wajasiriamali na Wainjilisti wanaalikwa kuwa wanachama wa chama hiki cha ATAPE. Chama hiki kina katiba inayokwenda sanjari na kanuni na sera ya kanisa na kila mwanachama anapaswa ajue Katiba hii ili aweze kutekeleza majukumu yake vizuri inavyotakiwa kwa manufaa ya kanisa kwa ujumla.

DIRA (VISION)

“Umoja ambao wanachama wake wanampenda Bwana kwa mioyo yao yote, akili zao zote na Roho zao zote” Mathayo 22:37

THANA (MISSION)

“Kutumia Vipaji vyote na Rasilimali zilizopo katika Kanisa kutangaza/kuhubiri neno la MUNGU kwa Mataifa yote” Mathayo 28:19-20

WALENGWA

i) Wanataaluma
ii) Wajasiriamali
iii) Watendaji wa serikali na mashirika
iv) Wanachama wa heshima
v) Wanachama walioshirikishwa (wanavyuo)

VIONGOZI WA ATAPE

We are committed to providing our customers with exceptional service while offering our employees the best training.

FREDDIE MANENTO

Mwenyekiti

JEREMIAH LIMA

Mhazini

JAMES LABAN

Katibu

MALENGO NA UMUHIMU WA ATAPE

Chama hiki ni cha muhimu. Hapa kuna baadhi tu ya mambo ambayo tunayoweza kuyataja kuonesha umuhimu wa chama hiki – kwa kanisa, kwa wanataaluma wenyewe na kwa washiriki kwa ujumla.

MALENGO YA ATAPE.

i) Kutambua na kuratibu talanta (taaaluma/ujuzi) zilizoko makanisani.
ii) Kukuza ushirikiano miongoni mwa waadventista wanataaluma na wajasiriamali
iii) Kutengeneza mazingira ya kuwafanya wakutane na kubadilishana mawazo
iv) Kuinua na kuimarisha maadili miongoni mwa waadventista wanataaluma na wajasiriamali
v) Kuwafanya wanataaluma na wajasiriamali watumie talanta zao kwa faida ya JAMII, KANISA na kazi ya Mungu, na kwa utukufu wa Mungu
vi) Kuwatia moyo kutumia vipawa vyao katika kulikuza KANISA na JAMII
vii) Kuwakumbusha kuwa wanadaiwa na WAKRISTO NA JAMII inayowazunguka, chochote cha ziada walicho nacho

UMUHIMU WAKE KWA KANISA.

i) Ulimwengu unabadilika, kanisa linahitaji wataalamu miongoni mwa washiriki wake ili kuliwezesha kanisa kukabiliana na mabadiliko mbali mbali ya ulimwengu wa sasa. Bila kuwatumia ipasavyo hawa wana taaluma mambo mengi ndani ya kanisa yanaweza kukwama.

i) Ulimwengu unabadilika, kanisa linahitaji wataalamu miongoni mwa washiriki wake ili kuliwezesha kanisa kukabiliana na mabadiliko mbali mbali ya ulimwengu wa sasa. Bila kuwatumia ipasavyo hawa wana taaluma mambo mengi ndani ya kanisa yanaweza kukwama.

i) Ulimwengu unabadilika, kanisa linahitaji wataalamu miongoni mwa washiriki wake ili kuliwezesha kanisa kukabiliana na mabadiliko mbali mbali ya ulimwengu wa sasa. Bila kuwatumia ipasavyo hawa wana taaluma mambo mengi ndani ya kanisa yanaweza kukwama.

i) Ulimwengu unabadilika, kanisa linahitaji wataalamu miongoni mwa washiriki wake ili kuliwezesha kanisa kukabiliana na mabadiliko mbali mbali ya ulimwengu wa sasa. Bila kuwatumia ipasavyo hawa wana taaluma mambo mengi ndani ya kanisa yanaweza kukwama.

UMUHIMU WAKE KWA WASHIRIKI

Wanataaluma na taaluma zao

Wanataaluma na taaluma zao ni rasilimali za thamani na muhimu sana kwa kanisa la Mungu. Kuwatumia ipasavyo sio tu kuokoa pesa na mali za kanisa lakini ni njia ya kulijenga kanisa na kuokoa roho za hao wanataaluma wenyewe. Tunao ushuhuda wa jinsi ambavyo chama hiki kimekuwa cha mbaraka na msaada mkubwa kwa washiriki wetu kupitia huduma zake.

Chama cha wanataaluma

Chama cha wanataaluma hutoa fursa kwa washiriki wenye taaluma mbali mbali kukutana na kufahamiana na kushiriki pamoja ujuzi wao katika mikutano ya ATAPE. Na hivyo katika mazingira hayo kufaidiana na kuendelea kukua kiroho, kiakili, kiuchumi na kijamii. Zingatia kuwa hakuna taaluma inayojitosheleza.

Huduma za malezi ya kiroho kwa wanataaluma

i) Talanta na ujuzi walio nao wamepewa na Mungu ili wazitumie kwa ajili ya utukufu wake. Wamepewa pia ili washiriki baraka za kuwa na vipawa hivyo na jamaa zao na jamii inayowazunguka kwa ujumla. Madai ya Mungu huja kabla ya madai yo yote yale.


ii) Kuwa na hizo talanta wanakuwa ni wadeni kwa wale ambao hawana au hawakujaliwa kuwa nazo.


iii) Kutumia hizo talanta kwa ajili yao na jamaa zao na ulimwengu na kusahau madai ya Mungu ya msingi ni dhambi kubwa.

Karakana ya kuwaandaa na kuwanoa hawa wanataaluma

Chama cha ATAPE kimekusudiwa kuwa karakana ya kuwaandaa na kuwanoa hawa wanataaluma kuwa mawakili waaminifu, watu wakutegemewa na kuwa msaada mkubwa katika kanisa la Bwana Mungu wao.

ATAPE KATIKA KAZI – KWA WASHIRIKI NA JAMII

Chama hiki hutekeleza majukumu yake kwa njia mbalimbali, hasa kupitia: Uinjilisti, Afya, Elimu na Ujasiriamali

UINJILISTI

Hili likiwa jukumu kuu la ATAPE, chama kimejikita katika kuunga mkono shughuli za kanisa na kuelimisha jamii maswala ya neno la Mungu kupitia:

> Ujenzi na uchangiaji wa nyumba za kuabudia takribani 11

> Usambazaji BURE wa vitabu vya neno la Mungu ambapo nakala zaidi ya 10,000 ikiwemo “pendo lisilo kifani” zimegawiwa BURE kwa jamii

> Mafundisho ya neno la Mungu kupitia RADIO NA TELEVISHENI za Hope Channel Tanzania (Morning Star), Star TV na mitandao ya Youtube, Facebook, Whatsapp na program tumishi (i.e. Mobile Apps).

> Idadi ya fedha ambayo imetumika hadi sasa kwa kazi hii ni zaidi Tsh 440,000,000 milioni

> Watu ambao wamefikiwa na neno ni zaidi ya 5,000,000

AFYA

ATAPE pia imeendelea kuwa mdau mkubwa wa kuunga mkomo huduma za afya kwa kutumia wataalamu wake wa afya na misaada ya kifedha na mahitaji ya wanachana. Katika hili, chama kimetenda yafuatayo:

> Kambi za afya, ambapo zaidi ya Watanzania 20,000 wamepata huduma za afya BURE kabisa

> Wataalamu wa afya zaidi ya 100, wamehusika katika kusimamia na kutoa huduma hizi katika vituo mbalimbali Nchini

> Pia chama kimeendelea kuunga mkono ujenzi wa vituo vya afya, hasa hospitali ya kanisa iliyoko mjini Mwanza

UJASIRIAMALI

ATAPE ni chama ambacho kimejikita katika kuwaleta pamoja wajasiriamali, wamiliki wa biashara, viwanda, wawekezaji na kuwajengea uwezo wote wenye NIA ya kuchangamkia FURSA. Katika hili ATAPE imefanya na inaendelea kufanya yafuatayo:

i) Kupitia Radio, TV, Mitandao ya kijamii na mafundisho ya hadhara, ATAPE imetoa elimu ya ujasiriamali BURE kwa washiriki na jamii ya watanzania, ambapo zaidi ya watu 5,000,000 wamefikiwa na wanaendelea kufikiwa na mafundisho/elimu hii ya ujasiriamali

ii) Ufunguaji wa FURSA za mashamba kwa wanachama wake. Ambayo yanatoa AJIRA kwa JAMII husika. Fursa hizi za mashamba ziko maeneo ya Mufindi – Iringa, Kwasunga – Tanga, Njombe, Ngerengere – Morogoro, Tomoni – Kibiti na Maji DSM

i) Mashamba haya yana ukubwa wa jumla ya hekari takribani 10,250.

i) Uwekezaji uliofanyika ni wa zaidi ya Tsh 1,039,000,000 milioni

Sekta ya elimu

Katika sekta ya elimu ATAPE imejikita katika:

i) Kutoa misaada ya ADA za kusomo kwa wahitaji katika jamii

ii) Kusaidia Kanisa katika mpango mkakati wa kudumisha elimu bora

i) Pia kutoa huduma ya KIROHO na mafunzo ya MAADILI katika mashule na wakati wa likizo

Mawasiliano

Tunapatinana taarifa za mawasiliano kama ifuatavyo.

Address

ATAPE

P.O.Box 1121

Arusha, Tanzania

E-mail

info@atape.co.tz

Mobile No.

0755202202 and 0784844949